Programu na akaunti
Ipi?
- YuMuuv inapatikana katika lugha zipi? YuMuuv inapatikana katika lugha zaidi ya 50, kuanzia Kialbania hadi Kivietinamu. Kila mshiriki huchagua lugha yake kwenye Taarifa zako; Kiaislandi na Krioli ya Haiti ndizo mpya zaidi.
- Programu inajifunga, inakwama au haifunguki Sasisha YuMuuv, ifunge kabisa kisha uifungue tena. Hatua zako zinabaki kwenye programu ya simu au saa yako, kwa hiyo hakuna kinachopotea wakati programu haifanyi kazi.
- Ninawashaje au kuzima arifa? Fungua Kikasha (chini kulia), gusa Mapendeleo (juu kulia) na uchague unachotaka kupokea. Ikiwa hupokei chochote kabisa, ruhusu pia arifa za YuMuuv kwenye mipangilio ya simu yako.
- Ninabadilishaje lugha ya programu? Gusa duara la wasifu wako (juu kulia), fungua Taarifa zako kisha uchague lugha yako. Lugha ya programu itabadilika mara moja.
- Changamoto yangu inaisha lini, na ninabadilishaje ukanda wangu wa saa? Kila changamoto inaisha saa sita usiku kulingana na ukanda wako wa saa. Matokeo yanaweza kuendelea kubadilika kwa hadi saa 72 baadaye wakati data iliyochelewa inasawazishwa.
- Ninabadilishaje anwani ya barua pepe ya akaunti yangu? Huwezi kuibadilisha kwenye programu. Wasiliana na timu ya usaidizi ukiwapa anwani yako ya sasa ya barua pepe na mpya, nasi tutakubadilishia.
- Ninawezaje kuacha kupokea barua pepe za YuMuuv? Sogeza hadi mwisho wa barua pepe na uguse Jiondoe.
- Je, ninaweza kutumia YuMuuv kwenye kompyuta yangu? Ndiyo. Nenda app.yumuuv.com na uingie kwa barua pepe na nenosiri unalotumia kwenye programu. Apple Health na Health Connect zinaweza kuunganishwa tu kupitia programu ya simu.
- NimetoZwa ada ya usajili wa YuMuuv. Ninawezaje kuughairi? YuMuuv haiwatozi watu binafsi ada kamwe; kampuni ndizo zinazolipia huduma. Ada hiyo imetozwa na kampuni nyingine, kwa hiyo angalia jina la mfanyabiashara kwenye taarifa yako ya miamala.