Msimbo wangu wa kujisajili haufanyi kazi
Ikiwa programu inasema Kagua tena msimbo wa kujisajili au wasiliana na mwandalizi kwa msaada, au inaonyesha “si sahihi” au “kikomo cha majaribio kimezidiwa”:
- Weka msimbo ukizingatia herufi kubwa na vistari kama ulivyoupokea, bila nafasi. Ni bora kuunakili na kuubandika. Usiongeze maneno au mwaka.
- Misimbo ya changamoto za awali huenda isifanye kazi tena. Angalia mwaliko wa hivi karibuni zaidi.
- Baada ya majaribio mengi ndani ya muda mfupi, majaribio zaidi huzuiwa kwa takriban saa moja, na hata msimbo sahihi huonyeshwa kuwa si sahihi. Subiri, kisha jaribu mara moja.
- Ikiwa unatumia Wi-Fi ya ofisini, jaribu data ya simu. Watu wengi wakijisajili kupitia mtandao mmoja wanaweza kusababisha kizuizi hicho.
- Sasisha programu iwe toleo la hivi karibuni zaidi.
Bado haifanyi kazi? Mwombe mwandalizi wako akague msimbo, au wasiliana na timu ya usaidizi ukiambatisha picha ya skrini inayoonyesha hitilafu.